Vifuu Vya Nazi
Vifuu vya nazi vilivyochomwa
Ungaa wa Mkaa
Unga wa Mkaa unaweza patikana kwenye mti wa mkuyu,kifuu cha nazi,msonobari na mkaratusi. unga huu unaweza saidia kutibu magonjwa yafuatayo:
- Kuumwa na nyoka
- Kiungulia
- Kusaga chakula
- Uvimbe
- Kutapika
- Kuharisha,kuhara damu
- Vidonda vya tumbo
- Matatizo ya Macho
- Kunywa Sumu
- Tindikali
Matayarisho
Kama inavyoonyesha kwenye picha,choma kifuu cha nazi hadi kiwe mkaa,saga uwe unga.Chukua kijiko 1 kikubwa cha unga wa mkaa changanya na maji safi ya kunywa ya uvuguvugu uwe kama uji uji, kikombe kimoja kunywa kabla ya kula.
Kwa mtu alieumwa na nyoka. Shona kifuko cha kitambaa cheupe,weka kijiko 1 kikubwa cha unga wa mkaa na maji kidogo,kisha mfunge sehemu aliyoumwa,pia anywe kikombe kimoja cha uji uji wa unga wa mkaa. Mpaka mfike hospital uwezekano wa sumu kua imekwisha ni mkubwa sana. Na kwa aliekunywa sumu anatakiwa kunywa kikombe kimoja cha uji uji wa unga wa mkaa kama huduma ya kwanza kabla hamjampeleka hospitali.
Imeandikwa na Dr. Jethro Kloods(Turejee Edeni)